Wanasaikolojia wamethibitisha kuwa ubongo wa binadamu kuna nyakati humsaliti, mara nyingi hutokea kwamba binadamu anapoangalia taswira yake kwenye kioo au picha yake, ubongo humfanya ajione mzuri mara tano zaidi ya jinsi alivyo kiuhalisia, imethibishwa kwamba ndio maana mtu akipiga picha ya pamoja na watu wengi hujihisi yeye ndio mzuri kuliko mwingine yeyote katika kundi la watu waliopo kwenye picha hiyo.

Tafiti za kisaikolojia pia zimebaini kuwa katika mazingira ya kawaida ya mwanadamu mwanaume husema uongo angalau mara sita kwa siku moja.

Pia tafiti nyingine zimebaini kuwa kwa mfumo huu wa maisha tunaoendanao, ifikapo mwaka 2020 wanawake milioni 142 chini ya miaka 18 watakuwa wameolewa.

Tafakari makini yaweza kuleta majibu sahihi juu ya ukweli au uongo kuhusu tafiti hizi, toa maoni yako juu ya tafiti hizi kwa kudhibitisha ukweli au uongo wa tafiti za wanasaikolojia.

 

Marekani yatoa wito kwa Qatar kumaliza mzozo na nchi za Kiarabu
Awekwa kwenye Jeneza akiwa hai na kutishiwa kuchomwa moto