Aliyekua mwamuzi wa michezo ya ligi ya nchini England Howard Webb amefichua siri za baadhi ya wachezaji wa klabu za soka nchini humo, kuelekea katika kipindi hiki cha sikukuu za mwishoni mwa mwaka.

Web amesema kuna baadhi ya wachezaji hufanya makusudi ya kutaka wapewe kadi za njano, ili wafanikishe azma ya kupumzika na kufanya mambo yao binafsi.

Mwamuzi huyo amefichua siri hiyo alipohojiwa na kituo cha televisheni cha BT Sports, ambapo alisema mara kadhaa aliwahi kukutana mtihani huo ambao hufanywa ndani ya uwanja.

Alisema wachezaji walikua akimfuata na kumtaka awaonyeshe kadi, hususan wale ambao walikua wanajua wanakabiliwa na orodha ya kadi nne za njano, hivyo walifanya juhudi za kusaka kadi nyingine moja ili wakose mchezo mmoja.

Hata hivyo mwamuzi huyo ambaye alijizoela umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wake wa uchezeshaji alidai kuwa, makusudi hiyo hufanywa katika michezo inayokaribia Boxing Day (Siku moja baada ya X-Mass).

Ligi ya nchini England imekua na utaratibu tofauti na ligi nyingine za barani Ulaya ambazo husimama kupisha sikuku za mwishoni mwa mwaka.

Kwa asilimia kubwa wachezaji wa ligi ya nchini England, huchukizwa na utaratibu huo kwa kuamini unawanyima nafasi ya kujumuika na familia zao ili kusheherekea sikukuu za mwishoni mwa mwaka.

Jose Mourinho: Messi Hang'oki Camp Nou
Wenger: Bado Tuna Nafasi Ya Kuongoza Kundi A