Mtazamo wa kikanda wa IGAD kuhusu janga la Chakula, umesema zaidi ya watu milioni 50 wanatarajiwa kukabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula kwa mwaka 2022 katika nchi saba za Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Uganda.

Mtazamo huo umesema, “Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, na Sudan zinakabiliwa na janga kubwa zaidi la chakula katika eneo hilo, kauli ambayo imeungwa mkono na Mashirika ya Umoja wa Mataifa FAO, WFP na IGAD mjini Addis Ababa, Ethiopia.

IGAD imesema takriban watu 300,000 wanatarajiwa kukabiliwa na Janga la njaa la juu ngazi ya nchini Somalia na Sudan Kusini mwaka huu 2022, huku hatari ya njaa ikitokea katika maeneo manane ya Somalia hadi Septembakwa kukosa uzalishaji wa mazao na mifugo, kuongezeka kwa gharama za chakula na kwa kukosekana kwa misaada ya kibinadamu.

Msaada wa chakula cha mtoto toka Shirika la Chakuloa Duniani, WFP.

Hali ya 2022, inaonesha watu milioni 50 hadi 51 wakitarajiwa kukabiliwa na Janga au njaa mbaya zaidi, inaashiria ongezeko kubwa kutoka mwaka 2021 wakati watu milioni 42 walikumbwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula.

Mwaka jana 2021, eneo la IGAD lilichangia karibu asilimia 22 ya idadi ya watu duniani katika Janga au njaa mbaya zaidi, huku takriban watoto milioni 10 walio chini ya umri wa miaka 5 wakikabiliwa na utapiamlo na asilimia 24 ya wakimbizi wa ndani milioni 51 duniani wakiwa katika nchi za IGAD, hasa Ethiopia, Somalia, Sudan Kusini na Sudan.

Katibu Mtendaji IGAD, Workneh Gebeyehu amesema, “mchanganyiko wa hali mbaya ya tabianchi, migogoro, na changamoto za uchumi mkuu hufanya iwe vigumu kwa jumuiya zetu kuhimili mitikisiko mingi na takwimu tunazotoa leo ni za kuhuzunisha, na nina wasiwasi zinaweza kuongezeka zaidi kwani matarajio ya msimu wa mvua wa Oktoba hadi Desemba ni mbaya.”

Mgao wa Chakula nchini Somalia.

LATRA, Polisi kutoa 'kibano' magari madogo ya Abiria
Serikali kufafanua sintofahamu nyongeza ya mishahara