Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda ndani ya jeshi hilo, huku aliyekuwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Suzan Salome Kaganda akiteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Mafao na Fidia Makao Makuu ya Polisi.

Wengine waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Murilo Jumanne Murilo ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ambapo kwa sasa amechukua nafasi ya (SACP), Suzan Kaganda Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.

Aidha, Nafasi ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Simon Sylverius Haule ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu wa Polisi wa Mkoa wa Mara

 

 

Video: Jerry Muro atema 'cheche' aiponda kamati ya maadili ya TFF iliyomhukumu
Dida Ajirudisha Young Africans