Katika harakati za kuzuia na kupunguza ajali za barabarani, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ya makamanda wa polisi katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

Mabadiliko hayo yamefanyika leo Julai 3, 2018.

Hata hivyo mabadiliko hayo yamechochewa na kauli zilizotolewa na Rais, John Pombe Magufuli jana katika hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwaapisha viongozi wapya walioteuliwa mara baada ya baadhi ya viongozi kuachishwa nyadhifa zao akiwemo, Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi na kulaumiwa vikali juu ya ongezeko la ajali pasipo kuchukua hatua yeyote.

 

 

Video: Mtoto wa Casto Dickson afariki dunia
Video: Pinda aupa tano mradi wa TACIP, 'Utaleta ukombozi kwenye sekta muhimu'

Comments

comments