Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza pamoja na Kamanda wa mkoa wa Pwani.

Katika mabadiliko hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, (DCP), Ahmed Msangi amekuwa Mkuu wa Kitengo cha Makosa dhidi ya binadamu, Makao Makuu ya Upelelezi jijini Dar es salaam, huku nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP), Jonathan Shana ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani.

Aidha, nafasi ya aliyekuwa Kamanda Polisi mkoa wa Pwani, imechukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Wankyo Nyigesa ambaye alikuwa Mkuu wa Oparesheni Kanda Maalum ya Dar es salaam.

Hata hivyo, taarifa hiyo imesema kuwa mabadiliko hayo ni kawaida kufanywa ndani ya jeshi la Polisi.

Hristo Stoichkov ahofia maamuzi ya Lionel Messi
Mwanaume: Usikubali kumwacha mwanamke mwenye tabia hizi

Comments

comments