Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa nchini.

IGP Sirro  amemhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nassiri kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba.

Taarifa hiyo ya mabadiliko imetolewa leo tarehe 3 Septemba, 2018 na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, ACP Barnabas Mwakalukwa.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa, nafasi ya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Nassir imechukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, SACP Mohamed Shehan Mohamed.

Hata hivyo, taarifa hiyo imeeleza kuwa, uhamisho huo ni mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya jeshi la polisi katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi, lengo kuu ni kufanya mabadiliko yenye tija kwa umma katika masuala ya ulinzi na usalama.

China kutoa dola bilioni 60 kusaidia Bara la Afrika
JPM ampa shavu Kaimu Meneja wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL)

Comments

comments