Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Nchini, Simon Sirro amepokea msaada wa magari manne yatakayotumika kwa shughuli mbalimbali za jeshi hilo.

Amepokea msaada huo mapema hii leo jijini Dar es salaam, kutoka kwa Kampuni ya utengenezaji magari ya Haval ya kutoka nchini China.

Aidha, Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Jianguo Liu amesema kuwa wameamua kutoa msaada huo wa magari ili kurahisiha utendaji kazi wa jeshi hilo.

Hata hivyo, Sirro ameishukuru Kampuni hiyo kwa kutoa msaada huo na kushirikiana na jeshi hilo katika vita ya kupambana na uhalifu.

Maaskofu wamkingia kifua JPM, wanena mazito kuhusu mimba mashuleni
Serikali yapunguza gharama za umilikaji ardhi