Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, amewataka wafanyakazi na wananchi wanaozunguka Mradi wa Reli ya Kisasa SGR kuacha kujihusisha na vitendo vya kihalifu na badala yake kutoa ushirikiano kwa Kampuni ya ‘Yapi Merkezi’ inayojenga mradi huo unaotumia fedha za ndani za Watanzania.

Ameyasema hayo wakati akifanya ziara ya kutembelea mradi huo unaoanzia kituo cha Ilala hadi Kilosa mkoani Morogoro, ambapo amesema kuwa kila mmoja anayo nafasi ya kufanya ili kuhakikisha mradi huo unamalizika kwa haraka na katika muda uliopangwa bila kuwa na vikwazo.

Aidha, amesema kuwa, Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha usalama unakuwepo wakati wote hata pale mradi huo utakapokamilika na kukabidhiwa kwa serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa, amesema kuwa kutokana na ziara iliyofanywa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini imewaongezea hali ya kufanyakazi saa 24 bila kuwa na hofu ya kiusalama kutokana na uwepo wa Jeshi la Polisi.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Machi 1, 2019
Video: Mfumo wa Ada Lipa wazidi kuwarahisishia watanzania ulipaji ada mashuleni