Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania IGP Simon Sirro, ametoa agizo kwa makamanda wa polisi Mkoa (RPC) na makamanda wa Polisi Wilaya (OCD) nchi nzima kuhakikisha wanapata muda wa kutembelea wananchi wao na kutatua changamoto zinazowakabili mtaani.

Ametoa agizo hilo leo katika ufunguzi wa kikao kazi cha maofisa waandamizi wa Polisi kinachofanyika jijini Dar es salaam.

“Wewe RPC kama haufanyi mikutano ya hadhara kwa wananchi wako unataka mpaka wakuletee matatizo yao hapo ulipo, kwanini usiende walipo? mkatatue matatizo yao kule, hivi na nyie ma RPC na ma OCD mnasubiri mpate dhamana? amesema IGP Sirro.

Aidha amelipongeza Jeshi la Polisi kwa ujumla kwa namna lilivyopambana na kukomesha mauaji ya raia yaliyokuwa yakitokea Wilayani kibiti, Mkoani Pwani.

“Habari ya Kibiti ndani ya Jeshi la Polisi haitofutika, ‘issue’ ilikuwa ni kubwa sana, lakini ‘slogan’ yetu ya umoja ndiyo nguvu yetu ndio imetufikisha hapa tulipo. sasa hivi ukizungumzia Kibiti hata viwanja vimepanda bei, wanasiasa wanafanya siasa zao ni heshima ya jeshi lakini pia ni heshima kwa vyombo vingine vya ulinzi na usalama” ameongeza IGP Sirro.

Pia amewataka maafisa waandamizi wa Jeshi hilo kufanya kazi kwa weledi pamoja na kusimamia sheria ikiwemo kuongeza mikakati ya kupunguza matumizi ya silaha na uhalifu.

Moto wateketeza Vichanga Wodini
Azam sasa kamili kuivaa Triangle Fc