Jeshi la Polisi Nchini limetakiwa kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia sheria na taratibu zitakazosaidia kujenga taswira chanya hasa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Hayo yamesmwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, alipokuwa akizungumza na askari na maofisa wa Mkoa wa Kagera, wakati wa ziara yake yenye lengo la kujitambulisha pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakati wakitekeleza majukumu yao.

Amesema kuwa, kila askari anajukumu mbele yake la kuhakikisha suala la uhalifu na wahalifu linadhibitiwa hususan kwa kuimarisha usalama wa raia na mali zao huku wakizingatia kuwa, mkoa huo unapakana na nchi jirani za Uganda, Rwanda na Burundi.

Katika ziara yake, Sirro amewahakikishia askari na maofisa kuwa, yupo tayari kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza na kuwataka askari kuongeza kasi ya kukabiliana na matishio ya kiuhalifu na wahalifu ili kuifanya jamii kuishi kwa amani na utulivu. 

Hata hivyo, katika ziara hiyo, masuala mbalimbali yamejadiliwa huku mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu katika mkoa huo pamoja na wilaya zake zikiibuliwa kwa kuzingatia kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

LIVE: Rais Magufuli katika ziara mkoani Kigoma
Ben Pol: Nimeshafanya kolabo na Chidima, sasa zamu ya Trey Songs