Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Jeshi la polisi katika uchaguzi wa mwaka huu 2020, halitarajii kutumia mabonu ya machozi kwani wanatamani uchaguzi uwe wa haki kama ambavyo Rais ameagiza.

“Tunataka uchaguzi wa mwaka huu uwe ‘credible’, uchaguzi ambao ni wa haki kama Rais alivyosema. Hatutaki ifikie mahala tuanze kutumia mabomu ya machozi” Amesema IGP Sirro.

Amewataka Wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na usalama za Wilaya na Mikoa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na kwamba hadi kufikia sasa hali ya usalama nchini imeendelea kuwa shwari na kwamba matukio ya uhalifu yamepungua.

Amesema hayo akiwa kwenye ziara ya ukaguzi mkoani Singida ambapo amewataka Polisi kuendelea kushirikiana na wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuacha kujiingiza kwenye matukio ya uhalifu hususan wa kutumia silaha za moto.

Aidha, amewataka baadhi ya wananchi ambao ni washtakiwa au wafungwa na wanaopata msamaha wa Rais kutoka gerezani, kuacha kujiingiza katika matukio ya uhalifu.

Sven atangaza safari ya ubingwa 2019/20
Tanzania yabaki na wagonjwa wa Corona wanne Pekee