Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Tanzania (IGP), Simon Sirro amesema mpaka sasa bado hawajambaini mtu aliyefanya shambulio la risasi kwa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu.

amesema ” sisi tunamsubiri Tundu Lissu aje afungue kesi, kitu gani kimetokea, mazingira gani  na yule dereva wake.Dereva tunamtafuta imekuwa shida, yeye mwenyewe alipopata matatizo yupo nje hatujamuona, tunamuona tu kwenye mitandao”

Katika hatua nyingine IGP Sirro amesema kuwa uchunguzi juu ya kupotea kwa mwandishi wa Habari za uchunguzi, Azory Gwanda wa gazeti la mwananchi unaendelea.

Ameeleza kuwa ameshafungua jalada la uchunguzi, na kuwataka watu kama wantaarifa kuhusu tukio hilo kuzifikisha polisi na si kuishia tu mtandaoni kwani haziwezi kusaidia.

Na amesisitiza kuwa suala la watu kupotea halijaanza leo huku akitolea mfano wa wazee wa kizanaki wengi walikuwa wanasemekana wamepotea lakini baadae wanaonekana.

Ronaldo ampigia 'debe' Pogba Juventus
Muweka hazina mbaroni kwa kutafuna mil.39 za kikundi

Comments

comments