Bamia ni mboga nzuri inayohusika na kutibu magonjwa mbalimbali katika ngozi ikiwa pamoja na kufanya ngozi yao iwe nyororo kutokana na uteute uliomo katika bamia ambao husaidia kuunda tishu za mwili na ngozi

Lakini pia bamia huusika kutibu chunusi ambazo limekuwa ni tatizo sugu kwa watu wengi ambao wamejaribu kutumia mkorogo wa kila aina na kudunda.

Chakufanya na bamia ili utibu chunusi , chukua bamia 5, limao 1 na maji kidogo.

Kisha chukua bamia zako zikatekate na uzisage kwenye chombo chako cha kusagia kama vile brenda, kisha chukua kipande cha limao na maganda yake na maji kidogo saga kwa pamoja.

baada ya kupata mchanganyiko huo paka usoni  hadi kwenye shingo acha kwa muda kisha bandua kama unavyoondoa maski nyingine usoni.

Inashauriwa kufanya kitendo hiki kwa muda wa siku tatu katika wiki.

Mbali na kufanya hivyo inashauriwa mtu kula bamia kwa wingi kwani bamia ina wingi wa vitamini A ambayo husaidia kutengeneza kinga ya sumu na madaktari wanasema kuwa sumu inapoingia mwilini bamia huzuia kusambaa kwake., na Vitamini A itokanayo na bamia husaidia kuupa mwili kinga ya kupigana na maradhi yatokanayo na virusi lakini pia kwa wale wenye matatizo ya kuona, bamia husaidia kuimarisha mwanga katika macho yako.

Wingi wa vitamini A huzuia maradhi yatokanayo na virusi kama vile mafua.

Ulaji wa mboga za majani kama bamia, husaidia katika kulinda mapafu na saratani za mdomo. Bamia zina wingi wa vitamini K ambayo husaidia kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu.

Auawa kwa kuoa mke wa pili bila kutoa taarifa
JPM: Haiwezekani wakulima wa korosho wakaendelea kunyanyasika