Mlinda mlango mashuhuri nchini Hispania Iker Casillas amekanusha taarifa za kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo.

Casillas ambaye bado anakumbukwa na mashabiki wa Real Madrid kufuatia mchango mkubwa alioutoa alipokua Santiago Bernabeu, amekanusha uvumi huo baada ya kuibuliwa kwa tetesi kupitia mitandao ya kijamii kuhusu kustaafu kwake.

Mlinda mlango huyo wa klabu ya FC Porto, amesema licha ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Hispania, Julen Lopetegui kutomuita kwenye kikosi kilichocheza michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, bado hajakata tamaa.

“Sijastaafu kuitumikia timu yangu ya taifa, sikuwahi kutangaza wala kumwambia mtu yoyote kuhusu taarifa za kustaafu,” Alisema Casillas alipozungumza na waandishi wa habari wa Ureno.

Picha: Mfalme Mohamed VI wa Morocco aweka jiwe la msingi ujenzi wa msikiti
Mchina aadhibiwa kwa kuuza bendera ya Zimbabwe