Ikulu ya Marekani imefuta kibali cha mwandishi wa habari wa kituo cha CNN muda mfupi mara baada ya majibizano kati yake na Rais Donald Trump.

Mfanyakazi wa Ikulu alijaribu kumnyang’anya kipaza sauti mwandishi, Jim Acosta wakati wa mkutano wa waandishi wa habari siku ya Jumatano.

Aidha, mkuu wa kitengo cha habari wa Kulu ya Marekani, Sarah Sanders amesema kuwa kibali cha mwandishi huyo kimefutwa baada ya kumshika shika mwanamke mmoja, madai ambayo yamepingwa na Acosta na kusema huo ni uongo.

Hali hiyo ilijitokeza mara baada ya Acosta kumuuliza swali Trump kuhusu hatua za hivi karibuni kuhusu maelfu ya wahamiaji wanaoelekea Marekani kutoka nchi za Marekani ya kati.

Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya CNN imesema kuwa hatua hiyo ya Ikulu ya Marekani ni ya kulipiza kisasi kutokana na maswali magumu ambayo amekuwa akiulizwa Trump na Jim Acosta.

Serikali yawataka wakulima wa zao la Korosho kuwa wavumilivu
Okwi, Pluijm watamba mwezi Oktoba