Mshambuliaji wa Klabu ya Mtibwa Sugar Cherles Ilamfya ameshangazwa na baadhi ya Mashabiki wa Soka la Bongo, wanaoonesha kushangazwa na hatua ya kuwa miongoni mwa Wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara waliopata kadi nyingi za njano msimu huu.

Hadi sasa Ilamfya ameoneshwa kadi Saba za Njano na Nyekundu moja, baada ya Klabu yake kucheza michezo Michezo 22 ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu za Mwadui FC, KMC FC na Simba SC amesema, adhabu hizo zimemkuta kutokana na kuipambania Mtibwa Sugar, na katu haziwezi kumtoa mchezoni pamoja na maneno ya baadhi ya Mashabiki.

Amesema hawezi kuacha mpinzani kuleta madhara kwa timu yao akamuacha apite bali atapambana naye na uamuzi wa Mwamuzi (Refa), ndio utaamua kama amecheza Rafu au vinginevyo.

“Kadi naipata kutokana na kupambania timu,haiwezi kunitoa mchezoni na siwezi kuacha mtu aende kufunga nimuache,kimsingi nashukuru kulinda kiwango changu kutokana na kufuata maelekezo ya kocha.” amesema Ilamfya

Kidunda, Tony Rashid kupanda ulingoni DAR
Sina kinyongo na yeyote: Tundu Lisu