Kiungo kutoka nchini Ujerumani Ilkay Gundogan, huenda akawa sehemu ya wachezaji wa kikosi cha Man City ambacho kitashuka dimbani mwishoni mwa juma hili, kuwakabili Man Utd katika muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya soka nchini England (PL).

Matarajio ya kiungo huyo aliyejiunga na Man City wakati wa majira ya kiangazi akitokea Borussia Dortmund kwa ada ya Pauni milioni 21 ya kucheza ktika mchezo huo, yameibuka kufuatia kupona majeraha ya goti la mguu wake wa kulia.

Gazeti la The Guardian la nchini England limeandika kuwa, Guardiola yupo tayari kumtumia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 katika mchezo dhidi ya mahasimu wake Man Utd, kwa lengo la kukazia idara ya kiungo.

Kama Gundogan atajumuishwa kikosini mwishoni mwa juma hili, atakua akicheza katika ligi ya nchini England kwa mara ya kwanza tangu aliposajiliwa miezi mitatu iliyopita.

Gundogan was accompanied by his parents in Manchester's city centreGundogan akiwa katika matembezi mjini Manchester, siku chache baada ya kusajiliwa na klabu ya Man City.

Mahasimu hao wawili wa mji wa Manchester, wanatarajia kupambana siku ya jumamosi huku wakiwa na kumbukumbu ya kuanza vyema msimu wa 2016/17, ambapo wote kwa pamoja wamefanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo yao mitatu iliyopita.

Mchezo huo pia utakuwa unawakutanisha Pep Guardiola na Jose Mourinho kwa mara ya kwanza kwenye ligi ya nchini England, lakini kwa kumbukumbu za miaka iliyopita inaonyesha waliwahi kukutana mara 17.

Katika kumbukumbu hizo Guardiola ameshinda michezo saba huku mpinzani wake Mourinho akishinda mitatu na michezo saba iliyosalia ilikwisha kwa matokeo ya sare.

Man City watamkosa mshambuliaji wao kutoka nchini Argentina Sergio Aguero ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu na chama cha soka nchini England (FA), baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga kiwiko kwa makusudi beki wa West Ham Utd Winston Reid.

Wachezaji wengine ambao wapo katika mashaka ya kucheza mchezo huo wa jumamosi ni Bacary Sagna pamoja na Vincent Kompany ambao bado utimamu wa miili yao haijawa sawa sawa.

Rekodi Ya Mark Clattenburg Na Manchester Derby
Eddie Howe Kumbadili Arsene Wenger?