Manchester City wametangaza kumsajili kiungo kutoka nchini Ujerumani Ilkay Gundogan kwa mkataba wa miaka minne.

Gundogan amejiunga na Man City, akitokea Borussia Dortmund kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 20 na amekua mchezaji wa kwanza kusajiliwa chini ya utawala wa meneja kutoka nchini Hispania Pep Guardiola.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, anaondoka Ujerumani akiwacha kumbukumbu ya kuwa sehemu ya kikosi cha Borussia Dortmund kilichotwaa ubingwa wa Bundesliga pamoja na kombe la chama cha soka DFB mwaka 2012, huku akichangia kuipeleka klabu hiyo katika hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2013.

Tanzania Yaporomoka Viwango Vya Ubora Duniani
Everton Wakorogana, Kila Mmoja Anamtaka Kocha Wake