Meneja wa Vinara wa Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ FC Barcelona Xavi Hernandez ameonyesha dhamira ya dhati ya kumsajili Kiungo kutoka nchini Ujerumani  na Klabu ya Manchester City, Ilkay Gundogan mwishoni mwa msimu kwa ajili ya kukiimarisha zaidi kikosi chakehicho.

Xavi anaweza kumpata kirahisi zaidi Gundogan kwa kuwa kiungo huyo anatarajia kumaliza mkataba wake ndani ya Man City mwishoni mwa msimu huu na anaweza kuondoka klabuni hapo akiwa mchezaji huru.

Gundogan mwenye umri wa miaka 32, amekuwa mtu muhimu ndani ya Man City tangu alipojiunga nayo mwaka 2016, na akiisaidia timu hiyo kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu ya England.

Kwa mujibu wa ripoti ya Athletic imebainisha kuwa Xavi anamuhitaji kiungo huyo ndani ya timu hiyo na tayari ameshamtumia ombi maalum.

Licha ya kuwa anaweza kupatikana akiwa mchezaji huru lakini FC Barcelona wanaweza kukutana na ugumu kumsajili nyota huyo wa Ujerumani kutokana na suala la tatizo la kiuchumi ambalo limewakumba timu hiyo.

Kocha Young Africans achukua tahadhari CAF
Folarin Balogun aipotezea Arsenal