Chama cha Ushirika na Mikopo cha Ilulu Saccos kilichopo Manispaa ya Lindi kimefanikiwa kupata jengo jipya la ofisi ambalo limegharimu kiasi cha Tsh. millioni 180.

Hayo yamesemwa mkoani humo na Mwenyekiti wa chama hicho, Hashimu Namwadilanga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa Ofisi hiyo ambapo amebainisha kuwa chama hicho kimeweza kupata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake hiyo ni pamoja na kupata jengo la ofisi za chama hicho.

Amewataka wanachama wa chama hicho kudumisha umoja walionao ili waweze kupata mafanikio mengi zaidi, Pia amevishauri vyama vya ushirika kushirikiana kwa pamoja ili waweze kupata mafanikio kama waliyonayo Ilulu Saccos

Naye Meneja wa Benki ya CRDB, Veronika Mashauri ameupongeza uongozi wa chama hicho kwa uamuzi wao wa kuwekeza katika kitega uchumi hicho kwani ni kitu muhimu kwa ustawi wa chama hicho.

“Hiki ni kitega uchumi muhimu sana, ukiacha tu jengo bado mna nafasi ya kufanya mambo makubwa huko mbeleni” amesema Mashauri

Kwa upande wake, Halfani Abdala Halfani ambaey ni mwanachama wa Ilulu Saccos ametoa shukrani zake za dhati kwa uongozi wa chama hicho kwa uamuzi huo wa busara wa kuweza kuwekeza katika kitega uchumi cha jengo hilo ambalo litaweza kuwaingiza mapato pamoja na kupunguza mzigo wa kukodi ofisi kama walivyokuwa wakifanya hapo awali. Chama cha ushirika cha Akiba na mikopo cha ilulu saccos kilianzishwa mwaka 2006 kikiwa na wanachama 152 ambapo hadi sasa kina zaidi ya wanachama 600 kikiwa na mtaji wa zaidi ya milioni moja.

Breaking News: Mwalimu ahukumiwa kunyongwa hadi kufa
Video: Mgonjwa wa Ukimwi aripotiwa kupona, Kusuka, kunyoa rufani ya Mbowe