Wakati waumini wa dini ya kikristu nchini wakiungana na mataifa mengine Duniani kusheherekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu kristu ambayo imekuwa ikifanyika desemba 25 kila mwaka.

Taharuki kubwa imetokea kwa wananchi wa kijiji cha Idunda kilichopo katika halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo mapema asubuhi siku ya tarehe 25 wa maandalizi ya kuelekea shughuli za ibada na kukutana na kifaa kikubwa kilichoanguka pembezoni mwa nyumba ya mmoja wa wanakijiji kikiwa kimefungwa pembe za ng’ombe mbele na nyuma.

Hali iliyowafanya wakazi wa kijiji hiko kuingiwa na hofu juu ya maisha yao na kuhusisha tukio hilo na imani za ushirikina.

Akizungumza kwa njia ya simu na mtandao huu mara baada ya kushuhudia tukio hilo mwenyekiti wa kijiji hicho Benedicto Erasto amesema kuwa dubwasha hilo lilianguka mara baada ya kushindana nguvu na mmoja wa wananchi anayeishi katika nyumba hiyo aliyefahamika kwa jina la Jino kwa Jino.

“Mimi nilivyoliona hilo dubwasha niliona pale linatisha nikaenda kumhoji mpangaji pale jana asubuhi nikamuuliza ilikuwaje akasema alivyolala usiku alisikia mtikisiko na akaona mwanga akaamka na kutoka nje kwa mujibiu wa vipimo vyao aliona sio kawaida akaingia ndani akachukua dawa akaanza kushindana nalo kulusha dawa akaona linashuka linapanda tena wakashindana kwa mda mrefu mpaka likatua chini kwa hiyo ndio akaondoka na kutoa taarifa ndio wananchi tukaanza kukusanyika”alisema mwenyekiti

Aidha mwenyekiti huyo amesema kuwa mpaka sasa hakuna madhara yeyote yaliyojitokeza na hivyo kwa sasa wanachosubiri ni kuona mwenye nyumba atatolea uamuzi gani juu ya dubwasha hilo.

Hata hivyo ili kujua ni jambo gani litakaloendelea baada ya tukio hilo ambalo linaendelea kuleta mshangao kwa wananchi kila wanapopita katika nyumba hiyo mtandao huu umemtafuta mmiliki wa nyumba hiyo ambaye inasemekana ni mpangaji na ni mganga wa tiba asili, ameshindwa kupatikana huku mwenyekiti wa kijiji hicho akieleza kuwa taarifa alizo nazo kwa sasa yupo safarini akitokea jijini Dar es salaam hivyo katika nyumba hiyo waliobaki ni wasaidizi wake wakimsubiri mkuu wao kwa maelekezo zaidi.

Kwa upande wake mmiliki wa nyumba hiyo bwana Joseph kabelege anayeishi mjini Njombe mara baada ya kutafutwa na mtandao huu anasema kuwa amepata taarifa hizo lakini kwa sasa hana cha kusema zaidi ya kumsubiri mpangaji wake aliyeko njiani akitokea Dar es salaam ili atolee maamuzi.

“Ninachofikiria chakufanya ni kumsubiri tu niliyempangisha kwasababu yupo safarini na yeye ndiye mwenye maamuzi kwasababu mimi nilimpangisha tu nyumba hivyo nasubiri akifika ndio liweze kutolewa na kesho nimeambiwa ndio wanalitoa”amezungumza kabelege huku akicheka.

Video: Mbowe atuma ujumbe mzito kutoka Segerea, ATCL yampa JPM majina ya vigogo
Maalim Seif kutimkia ACT- Wazalendo