Kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wazazi kuwalazimisha watoto wao kuoa au kuolewa kwa kisa wanachodai kuwa umri wao umeenda.

Tabia hiyo imewagharamu wazazi wa binti mmoja huko nchini Uganda ambapo binti huyo aliamua kufanya kitendo kilichoushangaza ulimwengu.

Binti huyo aliyefahamika kwa jina la Lulu Jemimah aliamua kujioa mwenyewe mara baada ya wazazi na ndugu zake kumlazimisha kuolewa kwa kipindi kirefu.

Lulu aliamua kuchukua uamuzi wa kujioa mwenyewe na kufanya hafla ndogo ambapo ilihudhuriwa na marafiki zake katika siku yake ya kuzaliwa mnamo Agosti,  27, 2018 ambapo alikuwa anatimiza miaka 32.

Licha ya hafla hiyo kuhudhuliwa na marafiki zake, Lulu alituma barua ya mwaliko kwa wazazi wake kuwataka wahudhurie sherehe hiyo waliyokuwa wakiisubiri kwa muda mrefu.

Lulu ni mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Oxford alifanya uamuzi huo mara baada ya kuchoka maneno yaliyokuwa yakizungumzwa kutoka kwa wazazi wake juu ya yeye kuolewa.

Hata hivyo Lulu amesema kwake kuolewa ni jambo la mwisho na sasa anasoma shahada ya udhamiri fani ya undishi.

 

Kim-Joung-un amwalika Papa
Msigwa mbaroni, apigwa 'stop' mikutano ya hadhara

Comments

comments