Wanaume wanne raia wa India waliofungwa kwa kumbaka na kumuua na mwanafunzi mjini Delhi mwaka 2012 wamenyongwa.

Akshay Thakur, Vinay Sharma, Pawan Gupta na Mukesh Singh walihukumiwa kifo na mahakama mwaka 2013.

Wanne hao walinyongwa katika gereza kuu la Tihar ikiwa ni mara ya kwanza hukumu ya kifo kutekelezwa India tangu mwaka 2015.

Muathiriwa alifariki kutokana na majeraha aliyopata siku kadhaa baada ya kubakwa na wanaume sita ndani ya basi.

Kisa hicho kilizua ghadhabu ya umma ambayo ilichangia kubuniwa kwa sheria mpya dhidi ya ubakaji nchini India.

Mwanafunzi huyo wa miaka 23, aliyepewa jina la Nirbhaya na vyombo vya habari kuashiria mjasiri hakuweza kutajwa jina lake halisi kwa mujibu wa sheria za India.

Katika miezi ya hivi karibuni, wafungwa wote wanne waliwasilisha ombi katika mahakama ya juu zaidi katika juhudi ya kutaka hukumu yao ibadilishwe kutoka kua kifo hadi kifungo cha maisha gerezani.

Lakini ombi lao lilikataliwa hatua ambayo iliwaacha bila njia nyingine ya kisheria ya kujinusuru. Rufaa ya mwisho ya kutaka hukumu ya kifo isitekelezwe dhidi yao pia ilikataliwa saa kadhaa kabla ya ya wote wanne kunyongwa.

Imeelezwa kuwa dakika kadhaa baada ya wafungwa hao kunyongwa Ijumaa asubuhi, mama yake muathiriwa alisema, “Nilitundika picha ya binti yangu ukutani na kumwambia hatimaye tumepata haki.”

Usalama ulikuwa umeimarishwa nje ya jela walikonyongewa wabakaji hao huku maafisa wa polisi wakipelewa kudumisha sheria.

Kundi la watu waliokuwa wamekusanyika nje ya lango la gereza hilo wakiwa wamebeba mabango walianza kusherehekea baada ya tangazo la kunyongwa kwa wafungwa hao wanne kutolewa.

Baadhi ya waliimba “kifo kwa wabakaji” na huku wakishukuru idara ya mahakama kwa haua hiyo.

Corona Kenya: Aiba fedha benki kwa madai ya kufanyia kazi nyumbani
Mwanajeshi mbaroni kwa kubaka wanafunzi watatu