Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles John Mwijage amepokea malalamiko kutoka India kuhusu utapeli uliofanywa na madali wa mazao kutoka Tanzania.

Hivyo taarifa kutoka India zinamtaka kwenda nchini huko kusafisha jina la Tanzania baada ya madalali hao kulichafua kwa kufanya utapeli.

“Nimepokea wito kutoka India kwa ajili ya kwenda kusafisha jina la nchi kutokana na taswira ilisababishwa uwepo wa matapeli hao,”alisema Mwijage.

Akifafanua zaidi, Mwijage ameeleza kuwa matapeli hao walifanya utapeli kwa kuwadanganya wafanyabiashara huko India kuwa wanapoagiza mazao wanapaswa kutoa pesa ya kianzio dola za Kimarekani 123,000 ambayo ni sawa na shilingi Mil.275 za kitanzania  na dola 200,000 ambayo ni sawa na Sh.448 mil za kitanzania.

Mwijage amekiri kupokea wito huo na amedai kuwa kampuni hizo za udalali zimechafua pakubwa jina la Tanzania na hivyo atahakikisha anawachukulia hatua kali za kisheria watuhumiwa hao ili kukomesha tabia hiyo na kuwa mfano kwa watu wengine wenye tabia ya utapeli.

Video: G Van atikisa na 'Kwako', Itazame hapa
Odinga aigomea tarehe ya marudio ya uchaguzi