Rais mpya wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Giann Infantino ameipa Afrika nafasi 5 za upendeleo zaidi katika ushiriki wa fainali za kombe la dunia mwaka 2026.

Katika fainali hizo timu zitaongezeka kutoka 36 hadi 48 na Afrika itawakilishwa na timu 9 ambapo nyingine ya 10 itapambana katika hatua ya mtoano.

Aidha, Shirikisho hilo pia limeongeza idadi ya timu kutoka katika bara la Ulaya ambapo mwanzoni zilikuwa ni timu 13 na sasa zitakuwa 16, huku Marekani Kaskazini na kusini zikiwa timu 6 badala ya 3.

Oceania nao wamepewa nafasi moja ya uwakilishi wa moja kwa moja ambapo hapo mwanzo iliwapasa wacheze mchezo wa mtoano na timu za Amerika Kusini ili kufuzu.

Hii itawafanya New Zealand kuwa na nafasi kubwa ya kushiriki kombe la dunia kila mara kutoka na kutokuwa na upinzani mkubwa haswa baada ya Australia kuanza kushiriki michuano ya bara la Asia.

Singida Utd Wamnasa Mwingine Wakimataifa
Mkoa wa Pwani wakabiliwa na upungufu wa vyumba wa madarasa