Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino ameipongeza Simba SC kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/2021.

Katika barua yake kwa Rais wa shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia, Rais Infantino amesema ubingwa ni matokeo ya juhudi na kutekeleza majukumu kwa kila mmoja ndani ya klabu hiyo.

“Naomba uwasilishe pongezi zangu kwa kila mtu aliyehusika katika mafanikio ya Simba SC, na kuwatia moyo ushirikiano, ari na ushupavu,” amesema Rais Infantino Katika barua yake.

Pia amemkshukuru Rais Karia na TFF kwa kuchangia maendeleo na ustawi wa Soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 17, 2021
Biashara Tanzania, Burundi kufikia Bilioni 200