Raisi wa Shirikisho La Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino ataendelea na majukumu yake kama raisi wa Shirikisho hilo,  licha ya uchunguzi wa mashtaka ya jinai kuendelea dhidi yake.

Juma lililopita waendesha mashtaka wa nchini Switzerland walifungua mashataka dhidi ya Infantino, kwa kile wanachokitaja ni kupanga na kukamilisha mkutano wa siri na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Switzerland Michael Lauber.

Mapema Julai, Michael Lauber alitajwa kushinikizwa kuachia ngazi, na kuchukuliwa hatua kutokana na madai ya rushwa yaliyoripotiwa, yanayowahusu yeye na raisi wa FIFA. Wahusika wote wawili wamekanusha madai dhidi yao wakati Luber akilazimika kujiuzulu wadhfa wake.

Wakati uchunguzi ukiendelea juu ya madai haya, FIFA wamesema hawajaona viashiria vya makosa yeyote. Vikao vilivyotajwa ni vikao vya kawaida na hawajaona sababu ya kuanzisha uchunguzi.

“Hakukuwepo na hakika hakuna sababu ya kufungua uchunguzi, hakuna kitu chochote kinachoashiria kufanyika kwa kosa la jina” -Sehemu ya tamko la FIFA.

Hata hivyo, Stefan Keller  ambaye alichanguliwa kuchukua nafasi ya Luber kama Jaji Mkuu amepitia madai hayo na amesema kuwa anaona viashiria vya makosa. Uchunguzi unatarajiwa kubainisha mengi ambayo yamejificha.

Wakati FIFA wakiona hakuna haja ya kumuwajibisha raisi wao, wanasema watatoa ushirikiano wa kutosha kwa vyombo vya uchunguzi katika kushughulikia suala hili. Kwa maana hii Gianni Infantino ataendelea na majukumu yake kama raisi.

Zitambue zitakazocheza FDL 2020/21
Wilfred Zaha aiogopa mitandao ya kijamii