Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Rais wa FIFA, Gianni Infantino atatua nchini Alfajiri ya Februari 22 kwa ajili ya kuongoza mkutano mkuu wa mwaka wa FIFA.

Taarifa iliyotolewa na Waziri Dkt. Mwakyembe imesema kuwa Rais wa FIFA anatarajia kuwasili nchini usiku wa saa nane kuamkia Februari, 22 2018 ambayo ndiyo siku ya mkutano na saa tatu asubuhi yake ataelekea Ikulu kukutana na viongozi wakuu wa nchi.

Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wilfred Kidao amesema mkutano huo wa viongozi wa FIFA na CAF umebeba ajenda mbalimbali ikiwemo kujadili maendeleo ya soka la wanawake, maendeleo ya soka la Vijana, Utaratibu wa kusaidia Vilabu vya soka pamoja na vipaumbele mbalimbali vya kukuza soka kwa nchi za Afrika.

Hata hivyo, Rais huyo wa FIFA anatarajia kuondoka nchini jioni mara baada ya kumaliza mkutano wake na kushiriki chakula cha jioni.

Chirwa awazodoa wanao mzushia
Wachezaji tisa walamba kadi nyekundu