Nyota wa Barcelona, Andres Iniesta leo ameweka wazi kuwa ataachana na klabu hiyo mwisho mwa msimu huu, huku akieleza kuwa hawezi kucheza dhidi ya Barcelona hivyo timu atakayoenda haiwezi kukutana na timu hiyo.

Iniesta ameyasema hayo baada ya mazoezi na wenzake huku akitokwa na machozi lakini alijikaza na kueleza mpango wake huo wa kuondoka katika klabu ambayo ameeleza ndio imemfanya leo dunia inamjua.

“Ninaposema naondoka simanishi ahadi yangu ya kutokuja kushindana na Barcelona nitaivunja, ni timu nayoiheshimu sana ndio maana sitaenda klabu yoyote ya Ulaya kwasababu sitaki kucheza dhidi ya Barcelona,” amesema Iniesta

Aidha, amesema kuwa Barcelona ni sehemu ya maisha yake na ipo siku atafanya nayo kazi tena japo hakuweka wazi ni kazi gani.

Hata hivyo, kiungo huyo aliichezea Barca mechi yake ya kwanza katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Club Brugge Oktoba 2002 akiwa na umri wa miaka 18. Hadi sasa tayari ameichezea mechi 669 katika mashindano yote na kuifungia mabao 57.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 28, 2018
Gigy Money ajifungua salama, hongera kwa kabinti