Nchini Rwanda, Taasisi ya Utetezi wa Haki za Wanawake (Profemmes Twese Hamwe) na Jukwaa la Waandishi wa Habari wa Kike nchini humo (ARFEM) wamepaza sauti kutaka muhubiri wa kanisa la kisabato, Niyibikora Nicholas kuchukuliwa hatua za kisheria baada ya kutangaza injili ya uchochezi akidai kuwa wanawake ni watu wabaya na chanzo cha matatizo, maovu na migogoro isiyoisha duniani.

Ofisi ya Mkuu wa mwendesha Mashtaka Rwanda imeliagiza jeshi la polisi kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai kuanza upelelezi juu ya madai yanayomkabili Mchungaji huyo.

Hata hivyo kituo cha radio ya dini cha Amazing Grace 105.1 FM kilisikika kikirusha matangazo ya mahubiri ya mchungaji huyo yaliyojaa uchochezi na chuki dhidi ya wanawake.

Hivyo Jeshi la polisi kitengo cha makosa ya jinai ya Rwanda kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Mawasiliano nchini humo (RURA), imekifungia kituo hiko cha redio ya dini cha Amazing Grace 105.1 FM kurusha matangazo kwa kipindi cha mwezi mmoja pamoja na kulipa faini ya faranga milioni 2 sawa na Tsh milioni 6.

Mchungaji huyo akiwa LIVE hewani amesikika akisema kuwa hata Mungu hawapendi wanawake, kwani mwanamke hajawahi kuwa mtu mwema tangu enzi za bustani ya edeni ambapo alikula tunda alilokuwa ameambiwa asile na kumshawishi na mumewe kufanya dhambi.

Mamlaka hiyo ilichambua mahubiri yake yote ambapo imeeleza kuwa maudhui yote yalitoa mifano lukuki ya kwenye biblia inayowaelezea wanawake kuwa ni watu wabaya huku mchungaji huyo akiwataka wanaume wasiwaamini wanawake kwani wanawake ni watu wabaya.

Mhubiri huyo alizua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii nchini Rwanda na kuwakasirisha wanawake.

Serengeti Boys kushiriki mashindano ya CAF-Cecafa Cup
Tamko la Zitto baada ya kutoka selo