Kocha Mkuu wa Simba SC Zoran Maki huenda akafanya mabadiliko kwenye kikosi chake leo Jumatano (Agosti 17), kwenye mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/23.

Simba SC itakua nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, ikiikaribisha Geita Gold FC ambayo inashiriki Ligi hiyo kwa msimu wa pili tangu ilipopanda Daraja Msimu wa 2021/22.

Kocha Maki anatarajiwa kufanya mabadiliko hayo katika eneo la ulinzi, ambalo linatajwa kuwa chanzo cha kupoteza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Young Africans, Jumamosi (Agosti 13) kwa kufungwa 2-0.

Katika mchezo huo Mabeki wa Kati walicheza Henock Inonga pamoja na Mohammed Outtara ambao walionekana kutokuwa na mawasiliano mazuri kwani wote wamezoea beki namba nne huku nafasi ya Kapombe ikichukuliwa na Israel Mwendwa.

Kocha Zoran amekiri mabeki hao wa kati (Inonga na Outtara) walifanya makosa ya kiulinzi katika mchezo dhidi ya Young Africans kushindwa kukaba vizuri, ameliona hilo na kuna mabadiliko makubwa ya kiuchezaji yanakuja.

“Katika eneo la beki wa kati kuna ushindani wa kutosha ila mazoezi ndio yanaweza kuamua kama Inonga na Outtara wanaweza kurudi kikosi cha kwanza au akacheza Joash Onyango, Kennedy Juma au Erasto Nyoni,”

“Wachezaji nilionao kila mmoja kwa nafasi yake akipambana na kujitoa kama majukumu yake yalivyo naamini watafanya vizuri, ingawa moja ya lengo letu kuchukua taji ya Ngao ya Jamii kushindwa kulifikia limetuuma.”

“Tunatakiwa kupambana ili kurudisha furaha kwa mashabiki wetu na hilo linawezekana tunaenda kupambana ili kuhakikisha tunafikia malengo yetu katika mashindano ya ndani yaliyobaki pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika, pia kutocheza kwa baadhi ya wachezaji ni kwa sababu hawakuwa fiti.” amesema Zoran

Kombe la dunia U17 hatihati kufanyika India
Uzalishaji chanjo ya kwanza ya Maralia Duniani mbioni kukamilika