Rapper mkongwe, Inspector Horoun aka ‘Babu’, amevunja ukimya kujibu tuhuma zilizoelekezwa kwake na mchumba wa Luten Karama anaefahamika kwa jina la ‘Bella’ kuwa humdhurumu na kumbania member mwenzako huyo wa Gangwe Mobb.

Inspector amefanya mahojiano na Bongo5 akiwa Afrika Kusini alikoenda kufanya show katika kipindi hiki cha sikukuu ya Eid.

Hiki ndicho alichoeleza Inspector:

“Kwanza nimesikitishwa sana kuambiwa mimi nambania demu wa Karama ( Isabella) pia nimesikia mimi nambania, nachukua show za Gangwe. Hizi habari nimezipata wakati nikiwa Afrika Kusini. Nimeshangaa sana kuona kwenye mitandao Isabella akinishutumu mimi,” amesema rapper huyo

“Nilikaa kimya kipindi kirefu kwa sababu watu wangu wa karibu waliniona na wakanishauri nikae kimya nisijibu lolote, lakini leo nimeona bora niongee ili kila kitu kiwe wazi ili watu wasije wakaona hizi shutuma ni za kweli. Mimi akina Luteni kwanza tuliachana mwaka 2002/3 ambapo Karama alijiengua kutoka la Gangwe Mob na kwenda TMK Wanaume Family na alikuwa anafanya kama msanii binafsi.

“Mimi nikakubali kuwa kama msanii wa kujitegema. Kwa kipindi hicho zilikuwepo tuhuma kama hizi lakini hazikufikia hivi na wakati huo alikuwa anasema simpi nafasi ya kusikika lakini baadaye alijiengua. Baada ya hapo mimi nilibaki msanii binafsi na pia naliwakilisha kundi la Gangwe Mob. Nikaendelea kama msanii wa kujitegemea, nikatengeneza albamu yangu ya kwanza ‘Pamba Nyepesi’ nikaja nikatengeneza albamu ya pili ‘Inabamba’, nikatengeneza albamu ya tatu Ndoa Haina Doa, kama msanii binafsi,”amefafanua msanii huyo.
“Kiukweli kabisa show nilizokuwa nafanya mimi sio za Gangwe Mob. Nina watu wangu wambao walikuwa wanahitaji kuirudisha Gangwe Mob baada ya mashabiki wetu kutaka tuirudishwe Gangwe, lakini haikuwa official kwamba Gangwe imerudi. Nawashanga wanavyosema nimefanya kazi za Gangwe na kuwazunguka au Karama na Bela au nambania Isabela. Hivi Isabela nambaniaje? Kwa akili ya kawaida tu, promoter anapiga simu mimi kwamba anataka Gangwe Mob, mimi nimwambie Luteni anakatazwa na mke wake au Bella anakatazwa na mume wake? Mimi sasa hivi nafanya kazi kutokana kazi zangu mpya, Kalama na Bella wanajaribu kujificha kwenye mwamvuli wa Gangwe Mob. Anajaribu kutoa hizi shutuma ili nionekane mimi ni mtu mbaya, jamii inielewe vibaya,”Anafafanua.

“Nakumbuka tulifanya kazi moja ya Gangwe Mob pale kwa Lamar ambayo tulimshirikisha Godzilla na wimbo ulikuwa unaitwa ‘Wabishi wa Kitaa’ lakini haikufanikiwa kufanya vizuri kwenye medani ya muziki na kurudisha kundi. Lakini kazi zangu binafsi zinafanya vizuri, kazi kama ‘Sharubu za Babu’ na zingine ambazo zimeamsha kazi za nyuma. Mimi nina albamu tatu mpaka sasa hivi na bado zina hit. Mimi niseme kwamba Gangwe Mob bora ibaki kuwa historia ili kuepuka mgogoro huu unaotokea. Mimi nasema uwanja uko wazi kama ana uwezo afanye kazi, afanye video kali, watu watamkubali, ni brand ana jina ni member wa Gangwe Mob, alifanya vizuri pia wakati tupo pamoja. Hii ni kujenga maneno fulani ambayo yanaumbwa ili kumbania mtu CV zake. Sijui alisikia nataka kutangaza nia ya kugombea ubunge! Sina nia hiyo ya kuingia kwenye siasa, wasinichafue kihivyo, mimi sina chuki nao,” amesisitiza Inspekta.

“Mimi sitaki kuamini kama sababu ya haya yaliyotokea si kumbania, kwa sababu Gangwe Mob bado haijarudishwa, bado hatujaanza kufanya kazi za Gangwe Mob, tulikuwa tunafanya kiushikaji ikitokea mtu anaihitaji Gangwe Mob mimi ndo namwita Kalama ‘ongea nao hawa’. Mimi nilimpa ruhusa kwamba ukipata mtu anahitaji show ya Gangwe Mob aelewane nao. Nilishaenda kufanya show ambazo yeye anaelewana na watu, sasa kuna kimoja labda kinaweza kuwa sababu kubwa. Kuna nyimbo ambayo tulifanya takribani miaka 2 iliyopita, nyimbo hiyo ilikuwa ya Isabela alimshirikisha Karama, akaomba anishirikishe na mimi kwa maana ya kuishirikisha Gangwe Mob. Nyimbo ya muda mrefu kidogo, imekaa karibia miaka 2, akasema tutafanya video kesho, kesho kutwa, siku zinaenda na kila mtu akawa anaendelea na shughuli zake.

“Baadaye baada ya kupiga piga show zao walikuwa wananiita kwenye show zao, siku nina nafasi naenda kwenye show zao na siku sina nafasi nawaambia naendelea na kazi zangu. Sasa nimewasaidia sana kwenye show zao, walikuwa wananipa pesa ya nauli tu, hakuna malipo yoyote lakini nilikuwa nachukulia poa kwa sababu ni watu wangu ambao najua hata mimi naweza nikawatumia kwenye kazi zangu. So baada ya kumaliza show tukaingia kwenye mwezi wa Ramadhani, huwa natulia tulia, nasoma, naswali kidogo nafunga sio mtu wa movement sana. Kazi kidogo nakuwa nimezisimamisha, siku moja ‘Jumatatu’ Karama akanipigia simu akaniambia tuna-shoot siku ya Jumatano, ile nyimbo ya Bela.
“Nikamwambia ‘mimi ule wimbo nimesahau mistari sasa tutafanyaje? Sitaki kumuangusha shem lakini mbona tumefanya ghafla hivi, sasa hivi kuna ushindani mkubwa sana watu wanafanya video wametulia wamejipanga’ akaniambia ‘bwana wewe njoo tu usipokuja tutumwangusha huyu shemeji yako atafeli’. Mimi nikamwambia huyo rafiki yangu itakuwa ngumu, mimi siwezi kuja kwenye hiyo nyimbo, kabisa siwezi kufanya, mimi siijui, sijajipanga kimavazi, ‘hoooo nguo zipo za kukodi’ nikamwambia ‘umekurupuka sana hauwezi ukaniambia leo Jumatatu Jumatano tunashoot video, halafu mimi sasa hivi nafunga ndugu yangu, wewe njoo huku huku tutajua kila kitu. Mimi nikamwambia , ‘katika hilo Karama utanilaumu, na unaweza ukanilaumu sana na shem, mimi sitoshiriki hiyo video kwa sasa hivi labda nyie m-shoot tu halafu vipande vyangu nita-shoot baadaye, hilo la kwanza.”

“La pili Karama alinipigia simu before kwenye chungu cha pili, tatu, kwamba kuna jamaa anataka tufanye show TCC Club Chang’ombe Eid Pili. Nikamwambia mimi tayari nimeshaongea na jamaa wa Afrika Kusini, nikamwambia kama huyo jamaa anaweza kuongea naye tusaini mkataba na atoe cash mapema kwa sababu hizi sikukuu ndo siku ambazo tunategema kupata income ya kuendesha maisha yetu japo tuna shughuli nyingine. Baada ya hapo akakaa kimya, hatujawasilana tena, mimi wakati huo tayari nimeshafanya mawasiliano na jamaa wa Afrika Kusini, nimeshaingia nao mkataba na tayari wameshatoa posters.

“Nikawatumia hata wao na pia nikaweka kwenye page zangu. Kama siku tano zimepita nikaona tangazo kwenye mtandao linasema ‘Gangwe Mob sijui watakuwepo Sigara, kwa maana hiyo unapotaja Gangwe Mob ni Inspekta na Karama. Yule promoter wangu wa Afrika Kusini akaniambia ‘mbona Inspekta tumeona tangazo utakuwepo Dar es salaam kupiga show na Gangwe Mob na sisi tumeshakupa pesa, kwanini unatuharibia? Nikawaambia ‘subiri msipaniki, hii siitambui, kama unataka kuamini kama siitambui naomba nizungumze na vyombo vya habari kukanusha hili, nikatangaza jamani eeh mimi sitakuwepo kwenye show ya TCC inayotangazwa labda member wangu Luteni Karama atakuwepo, lakini mimi sitokuwepo, msije mkaona mimi sipo mkaona mimi nimezingua, mimi nitakuwa na safari ya Afrika Kusini siku ya Eid, Eid Mosi na Eid Pili’.
“Baada ya kutangaza hivyo, nimekaa kama wiki ndo tayari nimepanga safari ya kuja huku, ndio hayo yaliyotokea. Lakini mimi sina ubaya nao.”

Tanzia: Banza Stone Atangulia Mbele Ya Haki
Dada Wa Lupita Nyong’o Akerwa Na Swali La Mhudumu Wa Hotel kuhusu Lupita