Mtandao wa Instagram utafanya jaribio la kuficha idadi ya waliopenda (likes) kwenye posti za intagram, ili kuondoa ule msukumo ambao watu wengi wanao wa kutaka kujua watu wangapi wamelike picha kwenye mtandao huo lakini pia kuufanya mtandao huo uwe sehemu ya kushirikisha mambo unayoyapenda.

Jaribio hilo linatarajiwa kuanza mapema Alhamis hii na katika nchi 6 ikiwemo Australia, Newzland, Ireland, Italy, Japan na Brazil.

Instagram imechukua hatua hiyo kupunguza mashinikizo ambayo yanafanya watumiaji kushindana mtandaoni ili wanachokiweka kipate idadi kubwa ya likes.

Ambapo picha ikishapostiwaa litaonekana jina la mmoja kati ya watu waliopenda picha hiyo na kisha wengineyo tofauti na awali ambapo idadi ya waliopenda picha au video ilikuwa inaonekana.

Mwanzoni mwa mwezi huu Instagram ilitangaza kuwa na mfumo mpya wa kukomesha udhalilishaji kwenye mtandao wake

Mwezi mei jaribio hilo lilianza kufanyika Canada na sasa linaendelea kufanyika nchi nyingine.

”Tunatarajia kuwa jaribio hili litasaidia kuondoa ile hali ya msukumo ya kutaka kujua picha yako itapendwa na watu wangapi, na kuufanya mtandao huo uwe sehemu ya kushirikisha mambo yako unayoyapenda tu na si ushindani wa kuangalia watu wangapi wamependa picha uliyopost” amesema Mia Galick Mkurugenzi wa Facebook Australia.

Instagram imesema jaribio hilo halitaathiri upande wa biashara kwani bado kutakuwa na uwezekano wa kuona orodha ya watu waliotazama picha au video kwenye mtandao huo kwa kubonyeza kitufe elekezi.

Amesema jaribio hili limeleta matokeo kwamba litasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza hali ya watu kujiamini kwani awali watu ambao walikuwa hawapati likes nyingi wamekuwa wakikosa kujiamini.

 

Fahamu namna mwili unavyofaidika na maji ya madafu
Askari 8 wa kesi ya madini wafutiwa kesi

Comments

comments