Ben Pol amekuwa mmoja kati ya mashahidi na watetezi wa faida za kutumia vizuri mtandao wa kijamii wa Instagram, baada ya mtandao huo kumuunganisha na mkali wa RnB kutoka Marekani, Ray J.

Kwa mujibu wa Ben Pol, hashtag ya jina la Ray J aliyoiweka kwenye kipande cha video kinachomuonesha akiimba ‘Quit Acting’ ambao ni wimbo wa zamani wa mwimbaji huyo akiwa na R Kelly ndio chanzo cha kupata dili ya kufanya naye wimbo.

Amesema kuwa baada ya Ray J kupitia hashtag zenye jina lake alikutana na kipande hicho cha video. Amesema Ray J alikipenda na kuamua kumtumia Ben Pol ujumbe wa moja kwa moja (inbox) akimshukuru kwa alichokifanya na kisha shukurani hizo zilizaa matunda mengine makubwa.

 

Mkali huyo wa ‘Phone’ ameeleza kuwa mawasiliano yao yalisababisha amtumie Ray J baadhi ya kazi zake, ndipo alipochagua kazi mbili mpya na kuingiza sauti yake kwenye moja kati ya kazi hizo.

Ben Pol aliiambia Sammisago TV kuwa anaendelea kuwasiliana na mkali huyo wa ‘I hit it First’ kuona uwezekano wa kuingiza pia maneno ya Kiswahili kwenye kazi ambayo aliichagua.

Ray

Ray J ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Kim Kardashian, ni mdogo wake Brandy na pia binamu wa rapa Snoop Dogg.

Wimbo wake ‘I hit It First’ wa mwaka 2013 ulifanikiwa kushika nafasi ya 51 kwenye chati ya ‘Billboard Hot 100’. Hivi sasa yuko kwenye maandalizi ya kuachia albam yake mpya ya ‘Raydiation 2’.

LIVE: Rais Magufuli akihutubia wananchi Tabora
Diva The Bawse: Nilidhani kiba angemuoa Jokate.