Klabu ya Inter Milan ya Italia imemsajili beki wa kushoto kutoka nchini Brazil na klabu ya Nice ya Ufaransa, Dalbert Henrique Chagas Estevao.

Dalbert mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na Inter Milan kwa mkataba wa miaka mitano kwa dau linalodaiwa kufikia Euro milioni 20.

Beki huyo anakuwa mchezaji wa sita kujiunga na klabu hiyo ya mjini Milan, katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi.

Waliomtangulia Dalbert ni Matias Vecin, Milan Skriniar Facundo Colidio, Borja Valero na Daniele Padelli.

Dalbert alijiunga na Nice msimu uliopita akitokea Vitoria Guimaraes ya Ureno. Akiwa nchini Ufaransa alicheza michezo 38, huku akiisaidia klabu hiyo kutinga hatua ya mtoano ya Europa League.

LIVE: IEBC ikitoa matokeo ya uchaguzi mkuu Kenya
Garry Monk: Ben Gibson Hauzwi