Rais wa Iran, Hassan Rouhani ameshutumu uvamizi wa mashambulizi yaliyoongozwa na Marekani nchini Syria akisema kuwa mashambulio hayo mashariki ya kati hayana athari zozote bali yanasababisha uharibifu.

Naye kiongozi wa kidini nchini Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amesema kuwa majeshi ya magharibi yanataka kuthibitisha uwepo wao katika eneo la mashariki ya kati kutokana na shambulio hilo.

Aidha, wakati huo huo wanachi nchini Syria wamefanya makongamano mbalimbali ya kumuunga mkono rais wa nchi hiyo wakisema kuwa walijua kuwa Marekani na washirika wake wataishambulia nchi hiyo, lakini wamesema hawaogopi kitu.

Hata hivyo, kwa upande wa waasi wanaopinga utawala wa rais Bashir Al Asaad wamesema kuwa mashambulizi hayo ya Marekani na washirika wake, hayatakuwa na maana yeyote kama hawata uondoa utawala wa Asaad.

Trump apigilia msumari Syria, ajipanga kuipiga tena
Fatma Karume aeleza atakachokipigania zaidi

Comments

comments