Iran imeituhumu Marekani kwa kusababisha kuongezeka kwa mvutano mkubwa na kusema kuwa serikali mjini Tehran inaendelea kujizuia kwa kiasi kikubwa licha ya Marekani kujiondoa katika mkataba wa nyuklia na madola mengine yenye nguvu.

Akizungumza jijini Tokyo nchini Japan ambako anafanya mazungumzo na maafisa wa Japan Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Mohammad Javad Zarif amesema kuwa hatua ya Marekani kuongeza mvutano huo haikubaliki.

Aidha, matamshi ya Zarif yamekuja saa chache tu baada ya Marekani kuaamuru wafanyakazi wake wasiokuwa na majukumu ya dharura kuondoka katika ubalozi wake wa Baghdad nchini Iraq kutokana na kile ilichosema kuwa ni kitisho kutoka kwa wanamgambo wa Iraq wanaoungwa mkono na Iran.

Hata hivyo, mvutano tayari ulikuwa mkubwa baada ya Rais Donald Trump kujiondoa katika mkataba wa nyuklia mwaka mmoja uliopita lakini umeongezeka zaidi katika wiki za karibuni baada ya Marekani kupeleka manowari zake za kivita katika Ghuba ya Uajemi kukabiliana na ilichodai ni vitisho vya Iran.

Spika Ndugai amkalia kooni Steven Masele, ‘huyu inabidi arudi nyumbani’
Video: Nelly asimamisha show yake baada ya mwanamke kumvua viatu

Comments

comments