Iran imesema kuwa iko tayari kuendelea na mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia iwapo Marekani itajitoa katika makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2015 kuhusu mpango wa silaha za nyuklia.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Javad Zarif ambapo amesema kuwa iwapo Marekani itajiondoa kutoka katika makubaliano hayo yajulikanayo kama JCPOA, basi nchi yake itaongeza kasi ya utengenezaji wa silaha za nyuklia.

Aidha, Rais wa Iran,  Hassan Rouhani alionya kuwa Marekani itajuta iwapo itajiondoa kwenye makubaliano hayo yaliyofikiwa kati ya nchi sita zenye nguvu zaidi duniani na Iran yanayolenga kudhibiti mpango wa kinyuklia wa Iran na badala yake nchi hiyo ilegezewe vikwazo vya kiuchumi.

Hata hivyo, Rais wa Marekani Donald Trump amezitaka nchi za Ulaya kufanyia marekebisho makubaliano hayo ifikapo tarehe 12 mwezi Mei mwaka huu kwa kuiwekea Iran mbinyo zaidi la sivyo Marekani itajiondoa kutoka katika makubaliano hayo yaliyofikiwa wakati wa utawala wa Barack Obama.

 

 

Yanga kutafuta pointi tatu kwa Mbeya City
Athari ya soda ndani ya dakika 20, 40, 180 katika mwili wa binadamu