Rais wa Iran, Hassan Rouhani amesema kuwa nchi yake itaendelea kutengeneza makombora ya aina mbali mbali bila hofu na katu hailazimiki kumuomba idhini yeyote kutekeleza azma yake hiyo.

Ameyasema hayo katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 40 ya mapinduzi ya Kiislamu yaliyo uangusha utawala wa Shah Mohammed Reza Pahlavi uliokuwa ukiungwa mkono na Marekani.

Amesema kuwa kamwe utawala wa nchi hiyo haitompigia magoti mtu yoyote au kuomba ridhaa ya mtu kuendelea na harakati zake za kujiimarisha kijeshi.

Katika hotuba yake, Rouhani imetilia mkazo kwamba njama zinazofanywa na adui dhidi ya Iran zitashindwa kwa namna zote, na kuonya kwamba sasa nchi hiyo ya Jamhuri ya kiislamu ina nguvu kubwa zaidi kuliko wakati ilipopambana na Saddam Hussein wa Iraq katika vita vilivyosababisha maafa makubwa na uharibifu kutoka mwaka 1980 mpaka 1988.

Aidha, amesema kuwa ulimwengu unapaswa kutambua kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  ina uwezo mkubwa zaidi kuliko siku za vita, pia ameipuuza miito kutoka Marekani na Ulaya ya kutaka pafanyike makubalino mapya ya kuzuia mpango wake wa Nyuklia.

”Mwaka huu tunasherehekea miaka 40 ya kinachoangaliwa kama siku ya ushindi katika mapinduzi ya kiislamu ya mwaka 1979 ya nchi yetu dhidi ya njama za wahalifu, Wamarekani,wazayuni na nchi zilizopitwa na wakati za kanda hii ambazo zinataka kuwaangusha watu wetu kupitia shinikizo na vikwazo. Leo uwepo wa umma mitaani katika sherehe hizi za kumbukumbu kote nchini kunamaanisha kwamba njama za maadui zimeshindwa. Uwepo huu unamaanisha kwamba adui hatofanikiwa katika malengo yake ya uovu,”amesema Rouhan

Hata hivyo, Rouhani ameipuuza miito kutoka Marekani na Ulaya ya kutaka pafanyike makubalino mapya ya kuzuia mpango wake wa Nyuklia., lakini kwa upande mwingine Kamanda wa ngazi ya juu katika jeshi la kimapinduzi la Iran amenukuliwa akisema nchi hiyo itaiangamiza miji ya Israel ya Haifa na Tel Aviv ikiwa Marekani itaishambulia jamhuri hiyo ya kiislamu.

 

Bandari Mpya yajengwa Muleba
Maelfu ya raia waandamana nchini Italy

Comments

comments