Mwenyekiti wa shirikisho la riadha nchini Kenya, Isaac Mwangi amesema anataka kujiuzulu kufuatia tuhuma za kuwahonga wanariadha ili kupunguziwa kifungo kutokana na utumiaji wa dawa za kusisimua misuli.

Mwangi, amekanusha tuhuma hizo na kusisitiza yu tayari kaachia nafasi yake kwa siku 21 ili kupisha uchunguzi unaoendelea kufanywa na shirikisho la riadha duniani.

“Tuhuma hizi zimenisababishia usumbufu mkubwa wa mawazo” Mwangi alisema”Ningependa jina langu lisafishwe”

Wanariadha wawili waliosimamishwa walidai Mwangi aliwataka kutoa fedha ili wapunguziwe adhabu, tuhuma ambazo Mwangi anasema hazina msingi.

The Game aahidi kumsaidia Kanye West $10,000,000 kwa masharti haya
Mayanja: Naujua Udhaifu Wa Yanga