Kundi la Kigaidi linalojiita Islamic States of Iraq and Syria (ISIS) limethibitisha kuwa mtu aliyewachoma visu watu 9 Jumamosi iliyopita katika duka kubwa la manunuzi huko Minnesota, Marekani alikuwa mwanajeshi wa kundi hilo.

ISIS wametoa tamko lao kupitia mtandao wa Amaq ambao unahusishwa na kundi hilo ambapo imeeleza kuwa hiyo ni sehemu ya harakati zake kuilenga Marekani na nchi za Ulaya kwa mashambulizi ya kushtukiza.

Aidha, mtu huyo aliyetekeleza tukio hilo alipigwa risasi na kuuawa na askari polisi ambaye hakuwa kazini muda huo.

Hata hivyo, Polisi wa Minnesota wamesema kuwa hawajathibitisha kama mtu huyo alikuwa akitekeleza tukio chini ya mwamvuli wa kundi lolote la kigaidi na kwamba wanachoamini hadi sasa ni mtu huyo alikuwa mshambuliaji wa kujitegemea.

“Hivi sasa tunajaribu kuingia kwenye undani wa tukio hilo kupata taarifa za chanzo cha chake,” Mkuu wa Polisi wa St. Cloud, William Blair Anderson aliiambia CNN.

Katika hatua nyingine, Marekani ilikumbwa na sintofahamu baada ya kutokea milipuko ya bomu katika eneo la Manhattan na kujeruhi watu 29 huku na bomu lingine likigundulika na kuteguliwa mapema.

Hakuna kundi lililotajwa kuhusika moja kwa moja na utegaji wa mabomu hayo.

Jeshi la Polisi latakiwa kuwatendea haki wananchi wanyonge
Video: Diamond Platnumz avaa viatu vya Saida Karoli