Aliewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismali Aden Rage amesema Simba ingeweza kuibuka na ushindi mnono kwenye mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Al Masry kama mchezo huo ungechezwa mapema.

Mchezo huo uliochezwa jana kwenye uwanja wa Taifa ulianza saa 12:00 jioni na ulimalizika kwa matokeo ya sare ya 2-2.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Rage amesema anaamini Simba ingeweza kuibuka na ushindi mkubwa kama mchezo huo ungechezwa saa 8:30 au saa 9:00 mchana.

Rage amesema zamani waliitumia mbinu hiyo ya kuwachezesha waarabu mchana wa jua kali hivyo kuwafunga kwa urahisi.

Bado nasikitika sana kwa jinsi nilivyoona Simba wamecheza vizuri, kama mpira ungechezwa saa 8:30 au saa 9:00 mchana wale waarabu walikuwa wepesi sana leo kwetu,” amesema Rage.

“Hizo ndio mbinu za mpira lazima ufanye mambo kwa kuangalia utafaidika vipi, huko nyuma tumewahi kushinda michezo mingi dhidi ya waarabu tunapocheza saa 8:30 au saa 9:00”.

“Nasema hivyo kwa sababu hali ya hewa ya Cairo sasa hivi ni nyuzi joto kati ya 7 hadi 8 na kwa vyovyote vile itakavyokuwa, sisi watatuchezesha usiku ambapo hali ya hewa itakuwa ni nyuzi joto 7 ambayo itatuathiri kidogo kwa sababu kutakuwa na ubaridi ambao hatujauzoea labda tuende mapema zaidi”.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa nchini Misri, March 16. Katika mchezo huo Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya kuanzia mabao 3-3 ili iweze kufuzu

Video: Upelelezi wa kifo cha Akwilina wafikia pazuri
Bashe ashindilia msumari hoja zake, “Rais amezungumzia mambo haya”