Wizara ya mambo ya ndani ya Israeli imesema kuwa itawaachia huru wahamiaji 200 kutoka barani Afrika huku kukiwa bado hakuna muafaka kuhusu kuhamishwa kwao pamoja na wengine kutoka Eritrea na Sudan ambao waliingia nchini humo kinyume cha sheria.

Israeli imekuwa ikijaribu kufanya mazungumzo na Uganda ikiitaka nchi hiyo ya Afrika Mashariki iwapokee wahamaiaji hao, ambao waliingia nchini Israeli kwa kuvuka mpaka wa Misri na nchi hiyo kwa miguu katika kipindi cha muongo mmoja uliopita.

Aidha, kwa upande wake waziri anayehusika na suala la majanga na wakimbizi nchini Uganda, Musa Ecweru amesema kuwa nchi hiyo inafanya mazungumzo na Israeli kuhusu suala hilo, lakini akasema kuwa itawapokea wakimbizi ambao wataondoka Israeli kwa hiari yao na wala siyo kwa kulazimishwa.

Hata hivyo, Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR, imesema kuwa Waafrika 4,000 waliokuwa wakitafuta hifadhi, wameondoka nchini Israel kwa hiyari na kuelekea Uganda na Rwanda tangu mwaka 2013, ripoti ambayo Uganda na Rwanda zimekanusha.

 

 

Karume Boys wafukuzwa Bujumbura
Simba SC kuwakabili maafande wa jeshi la Magereza

Comments

comments