Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema kuwa nchi yake itachukua hatua kali dhidi ya Iran, na washirika wake wa mashariki ya kati, huku akisema kuwa Tehran ni tishio kubwa kwa dunia.

Ameyasema hayo katika mkutano wa usalama unaofanyika mjini Munich, ambapo amesema kuwa Israel  haitauruhusu utawala huo kuweka kitanzi cha ugaidi katika shingo.

Akihutubia  katika mkutano wa usalama mjini Munich kwa mara ya kwanza, Netanyahu amewataka maafisa wa   Marekani na Ulaya waliokusanyika pamoja na wanadiplomasia kupambana na Iran haraka.

Hata hivyo, amesema kuwa Iran inaongeza nguvu zake wakati muungano unaoongozwa na Marekani dhidi ya  kundi linalojiita Dola la Kiislamu nchini Iraq na Syria unakomboa maeneo kutoka kwa wanamgambo hao.

Video: Mauaji ya mwanachuo yavuruga Polisi, Wazazi watoa neno zito
Mashambulizi ya Marekani yaua wanajeshi wa Urusi