Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameituhumu nchi ya Iran kuwa inajenga viwanda vya makombora ya nyuklia nchini Syria na Lebanon kitu ambacho amesema kuwa kitahatarisha amani ya mashariki ya kati.

 Netanyahu amesema kuwa mchezo huo inaoufanya Iran sio kitu kizuri kuzifanya Syria na Lebanon kuwa kituo chake kikuu cha kutengeneza vifaa vya kijeshi kama mpango wake wa kutaka kuiangamiza Israel.

Aidha, Majeshi ya Iran yanamsaidia Rais wa Syria, Bashar al Assad katika vita vilivyoshamili nchini humo huku ikiliunga mkono kundi la wapiganaji wa Lebanon la Hezbollah ambao wamekuwa wakihatarisha amani ya mashariki ya kati.

Hata hivyo,  Netanyahu ametoa matamshi hayo muda mfupi mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutterrez mjini Jerusalem.

Video: Kichupa cha Patoranking na Diamond Platinumz 'Love you Die'
Kamati ya Bunge yafanya ziara Muhimbili, Dart na IFM