Israel imewakamata viongozi waandamizi wa Palestina, ikiwa ni pamoja na Gavana wa eneo la Jerusalem linalomilikiwa na Palestina, Adnan Ghaith.

Israel imethibitisha kuwashikilia viongozi hao waandamizi kwa siku nne hadi leo; na kwamba wanaendelea kuwahoji, tukio ambalo limetafsiriwa na Palestina kama utekaji na uhalifu dhidi ya viongozi wao.

Mbali na Gavana huyo, kiongozi mwingine aliyekamatwa ni mkuu wa kitengo cha intelijensia cha eneo hilo. Israel ambao hawakutoa maelezo ya kina wamesema kuwa wanaendelea kuwahoji katika makao makuu ya jeshi la polisi yaliyoko Jerusalem.

Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na vyombo vya usalama vya Palestina, Ghaith ‘alitekwa’ na polisi wa Israel waliosimamisha gari lake na kumchukua wakiendesha kuelekea eneo lisilojulikana.

Kwa mujibu wa Wafa, kiongozi huyo alikamatwa karibu na kizuizi cha jeshi la Israel katika kijiji cha al-Judeira, Kaskazini-Magharii mwa Jerusalem.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa kukamatwa kwa viongozi hao kuna uhusiano na tukio la utekwaji wa mtu mwenye asili ya Palestina ambaye anafanya kazi na jeshi la Israel.

Mtu huyo anadaiwa kuwa na kitambulisho cha Israel pamoja na uraia wa Marekani na hufanya kazi na mataifa hayo yenye ushirika wa karibu.

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 22, 2018
Video: Ndege zenye nauli ya gharama zaidi duniani, hadi milioni 120 kwa kichwa

Comments

comments