Mshambuliaji mwenye uraia wa Niger huenda akatangazwa wakati wowote na uongozi wa klabu ya Yanga baada ya kutua nchini kimyakimya usiku wa Jumanne.

Mchezaji huyo Issoufou Garba anaendelea kufanyiwa majaribio na kocha Hans van de Pluijm ili kuangalia uwezekano wa kumpa mkataba pale jangwani.

Alizaliwa February 2, 1990 kwenye mji wa Niamey, Niger amewahi kupita kwenye vilabu kadhaa lakini hata hivyo hakupata nafasi ya kucheza kwenye vilabu hivyo.

Yanga inakabiliwa na michuano ya kimataifa ikiwa inatarajiwa kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika mashindano makubwa kwa upande wa Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Garba amepita kwenye timu kadhaa lakini timu yake ya kwanza kuitumikia ilikuwa ni AS FAN ambako alijiunganayo mwaka 2010 lakini hakupata nasafi ya kucheza hata mchezo mmoja kwenye timu hiyo hadi alipojiunga na klabu ya Muangthong United ya nchini Thailand ambako pia hakupata nafasi ya kucheza mchezo hata mchezo mmoja.

Mambo hayakuishia hapo, mchezaji huyo akaendelea na safari yake ya kutafuta mafanikio katika soka ambapo mwaka huohuo alijiunga na klabu ya Phuket ambako alikaa hadi mwaka 2012 bila kucheza hata mchezo mmoja kwenye timu hiyo.

Mwaka 2012 alijiunga na klabu ya Club Africain lakini bado jinamizi la kutopata nafasi ya kucheza kwenye vilabu alivyojiunga navyo lilizidi kumwandama kwani hata kwenye timu hii bado hakupata nafasi ya kucheza hata mchezo mmoja. Mwaka huohuo akasajiliwa na klabu ya ES Hammam-Sousse lakini bado hali iliendelea kuwa tete kwa mchezaji huyo kutokana na kuendelea kusugua benchi.

Mchezaji huyo ameitumikia timu yake ya taifa ya Niger katika mechi 17 katika kipindi cha mwaka 2011 na kufanikiwa kufunga magoli mawili (2) lakini bado haijafahamika kama bado anaendelea kuitumikia timu yake ya taifa hadi leo.

Katika kipindi cha usajili wa dirisha kubwa klabu ya Yanga ilimsajili mchezaji Joseph Tetteh Zuttah lakini mchezaji huyo alishindwa kuonesha makali kwenye kikosi hicho mwisho wa siku akapigwa chini.

Siku chahe zilizopita uongozi wa Yanga ulivunja mkataba na Andrey Coutinho kwa madai kwamba kiwango chake kimeshindwa kumvutia mwalimu wa timu hiyo Hans van Pluijm.

Swansea City Wamtimua Garry Monk
Magufuli ataja Baraza lake la Mawaziri, Orodha ya wateuliwa iko hapa