Muuguzi wa Chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) katika Hospitali ya San Gerardo, Daniela Trezzi (34) amejiua baada ya kupata maambukizi ya virusi vya Corona na kuhofia kuwa atawaambukiza wengine.

Mbali na hofu ya kueneza Virusi hivyo, imeelezwa kuwa Daniela pia alikuwa na msongo wa mawazo uliosababishwa na kazi kubwa wanayofanya watumishi wa afya katika kudhibiti vitusi hivyo.

Kabla ya kifo chake aliwaambia wafanyakazi wenzake kuwa ana wasiwasi amemuambukiza mtu mwingine Virusi hivyo.

Imeelezwa kuwa zaidi ya wahudumu wa hospitali 2600 wameambukizwa virusi hivyo ambao ni zaidi ya asilimia 8 ya wangonjwa wote nchini Italia.

Uchunguzi zaidi wa kifo cha muuguzi huyo unaendelea huku hali ikieendelea kuwa mbaya nchini Italia baada ya nchi hiyo kutangaza vifo vya watu 7503 ambapo vifo 683 vikiripotiwa kwa saa 24 zilizopita.

Video: Vipimo corona vyanasa mgeni mwingine Zanzibar, Mafuriko yaivuruga Rufiji
Corona Kenya: Wafungwa waachiwa kupunguza msongamano

Comments

comments