Kiungo kutoka nchini Croatia Ivan Rakitic amesema ana ndoto za kucheza soka chini ya utawala wa meneja wa Man City Pep Guardiola.

Rakitic ambaye kwa sasa anaitumikia FC Barcelona hakuwahi kucheza chini ya utawala wa meneja huyo ambaye alifanya kazi Camp Nou kwa mafanikio makubwa.

Amesema anavutiwa na utendaji kazi wa Guardiola na anaamini ipo siku watakutaka katika kapu moja na kufanya kazi ambayo italeta mafanikio kwenye soka lake.

Hata hivyo Rakitic, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Barca ambacho hii leo kitakua ugenini kikicheza mchezo wa hatua ya makundi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Man City.

“Nina matumaini makubwa ya kucheza chini ya utawala wa Guardiola katika siku za maisha yangu ya soka, Najua itakua hivyo kutokana na maisha ya sisi wachezaji kutotegemea sehemu moja kucheza soka.

“Nilichagua jezi namba 4 ya FC Barcelona kwa sababu yake, kwani natambua alivyokua akicheza Camp Nou alivaa jezi namba 4, ambayo ninaamini mpaka hii leo bado anaipenda na kuitazama pindi ninapokua uwanjani.

Image result for ivan rakitic jersey

“Pep ni mmoja wa wadau wa soka duniani, ninaowahusudu sana, na daima nitaendelea kumuombea kwa mungu ili afanikiwe zaidi katika kazi zake za ukufunzi.” Alisema Rakitic alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili England.

Nana Kwaku: Jose Mourinho Amuombe Radhi Eva Carneiro
Arsenal Yaacha Wanne Safari Ya Bulgaria